Elias Pirianoy

Fisi akivuka ziwa

Mnyama
Fisi
Kwa Kiingereza
Spotted hyena
Jina la kisayansi
Crocuta crocuta
Mahali
Ndutu, Serengeti

Umevutiwa na picha hii?

Faili la kidijitali ni la ukubwa kamili, kwa matumizi binafsi: lichapishe kwa ukubwa wowote au lionyeshe nyumbani. Kwa machapisho, bei inategemea matumizi.

Kutoka porini

Ilikuwa ni muda wa asubuhi, nilipokuwa naendesha kwenda nje kutafuta wanyama. Nilikuwa naelekea ziwani, Ziwa Ndutu, huko kusini mwa Serengeti. Ndipo nikakutana na mzoga wa nyumbu aliyekufa pembezoni mwa maji, na hapo hapo kulikuwa na fisi wengi sana wakila mzoga huo.

Ndipo nikamwona fisi mmoja akikatiza katikati ya maji akiwa na mguu wa mzoga huo, akikimbia kwenda kuuhifadhi mahali ili aule baadaye. Ni moja kati ya matukio mazuri sana niliyowahi kuona, kwani wanasema mwenye nguvu ndiye atakayechukua chakula, lakini mwenye legelege kidogo pengine ni ngumu.

Nisikilize nikisimulia (kwa Kiswahili, 1:09)